Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa kurudisha hadhi ya zao hilo nchini.

Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80 elfu  Mwaka 2017 na Tani laki moja  Mwaka 2021.

Katibu Mkuu amemuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini  chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.