WADAU wa sekta ya Ardhi nchini wameiomba serikali kuharakisha mpango wa upimaji wa matumizi sahihi ya ardhi katika maeneo ya ufugaji na kilimo kama njia mojawapo itakayosaidia kupunguza migogoro ya ardhi isiyokoma  ambayo imekuwa ikisababisha uvunjifu wa amani

Kauli hiyo wameisema  jijini Arusha katika mkutano wakubadilishana uzoefu ulioandaliwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya VSF Belgium yenye makao yake makuu mkoani Arusha,inayojishughulisha na mpango wa matumizi bora ya Ardhi .

 

Wadau hao wameieleza serikali umuhimu wa kutoa kipaumbele katika sekta ya ardhi  kwa kutenga bajeti ya kutosha ili kukamiliza mpango wa upimaji wa matumizi  bora ya ardhi kwenye vijiji zaidi ya 12,500 vilivyopo hapa nchini

Kwa upande wake afisa mipango kutoka tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi, Jerald Mwakipesile , alisema kuwa changamoto ya migogoro ya ardhi hapa nchini imekuwa ikiongezeka kwa sababu vijiji vingi havijapangiwa mpango wa matumizi sahihi ya ardhi.