Watu wapatao 14 wameuawa baada ya washambuliaji wanne wa kujitoa muhanga kujilipua kwenye mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, ambako magaidi wa Boko.

Haram wamesababisha mamilioni ya wakimbizi wa ndani na ambako pia wameshawaua watu takriban alfu 20. Polisi wamesema mashambulio hayo yalitokea wakati wa sala ya jioni.

Polisi wamefahamisha kuwa washambuliaji hao wanne pia waliuawa. Wawili walikuwa wanaume na wawili walikuwa wanawake.

Kundi hilo la kigaidi linaloendesha upinzani kwa karibu miaka kumi sasa halijasema iwapo lilifanya mashambulio hayo.