Aliyekuwa mshindi wa michuano ya Wimbledon mwaka 1998 raia wa Uswisi Jan Novotna amefariki dunia jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kansa kwa muda mrefu.

Katika enzi za uhai wake Novotna amewahi kuingia katika fainali moja ya Australian Open na French Open, huku akiingia fainali za Us Open mara mbili na akifanikiwa kushinda grand slam 12.

Novtana atakumbukwa kwa ubora wake miaka ya 90 akishinda makombe binafsi 24 tangu aanze tennis.

Mwaka 1997 Novtna alipoteza katika michuano ya Wimbledon kwa kutolewa na Marina Hingis lakini mwaka mmoja baadae ilipofika 1998 alilipa kisasi kwa kumtoa Hingis katika nusu fainali kisha kumshinda Nathalie Tauzat katika fainali.