Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro kuitikia wito wa jeshi hilo.

Heche amefika kituoni hapo jana Jumatatu Novemba 20,2017 saa sita mchana.  Wakati Heche akiwa kituoni hapo baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema wa Manispaa ya Morogoro walionekana wakizunguka maeneo ya kituo hicho.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema Heche aliahidi kwenda kituoni hapo.  Mbunge huyo alisema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa alipomsindikiza mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali alipotoka gerezani.

Akizungumza Jumamosi Novemba 18,2017 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara wilayani Kilombero Aprili 8, 2017.