SHULE BORA
Shule ya bweni  kwa wasichana na wavulana iliyopo llboru mita 800 toka barabara ya Moshi-Arusha katika jiji la Arusha. Tunakukaribisheni nyote kujiunga na shule pendwa kwa masomo ya kidato cha kwanza 2018 na nafasi chache za kuhamia kwa kidatocha II ,III na- V
MASOMO YA 0-LEVEL
Tunafundisha masomo ya sayansi, biashara na sanaa ambayo ni Hisabati, Fizikia, Kemia, Baiolojia, Jiografia, Biashara, Bookkeeping, Historia, Kiingereza, Kiswahili na Uraia. Pia Winning Spirit ni kituo kilichosajiliwa na baraza la mitihani NECTA cha mitihani ya maarifa (qualifying test QT) na watahiniwa binafsi (Private candidate PC).
Wanafunzi wote wa QT na PC wanakaribishwa kujiunga na shule kwa nafasi chache zilizopo.
MICHEPUO KWA A-LEVEL –
Tunafundisha michepuo ifuatayo;
PCM, PCB, CBG, PGM, EGM, ECA, HGE, HGL, HGKna HKL

Michepuo tajwa hapo juu humuandaa mwanafunzi kuwa mwananchi mwajibikaji ambaye ataajiriwa kwenye sekta mbalimbali au kujiajiri.

WINNING SPIRIT
Lengo letu ni kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu kwenye mazingira salama, yenye amani, nidhamu na mazuri kitaaluma. Kikosi chetu cha waalimu bora wenye wito, mafunzo na uzoefu wa hali ya juu wapo wakiwa na nia moja ya kuwalea na kuwafunza vijana

FOMU ZA MAOMBI YA KUJIUNGA zinapatikana kwenye tovuti
http://winningspirithighschool.ac.tz AU Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba
0784 64 64 46 , MENEJA – 0754381844, MKUU WA SHULE – 0766 657959/0788 657959 Winning spirit high school , P. O. Box 11064 , ARUSHA

KWANINI WINNING SPIRIT?
1. Winning Spirit ina waalimu na wafanyakazi wasio waalimu ambao kwa pamoja wana wito, maono, uvumilivu na nia ya dhati kuhakikisha mwanafunzi anaelimika na kuleta matokeo chanya katika maisha yake. Pia kuna patron na matron kwa ajili ya wanafunzi wa bweni ambapo matron ni muuguzi (nurse) kitaaluma kwa ajili ya wanafunzi watakaougua. Kunapokuwa na ulazima mwanafunzi hupelekwa hospitali kwa huduma zaidi. Kwa ufupi ni kuwa mwanafunzi wa Winning Spirit yuko katika mikono salama.

2.Adazetuninafuu. Nyenzo(facilities)zaWinningSpiritniza hali ya juu kwa mfano jenereta la tahadhari, kisima cha maji safi, ICTfacilities, nk. ambazo zingeweza kusababisha ada itozwe kiasi kikubwa zaidi ila imekuwa kinyume chake.

3.Winning Spirit ni shule inayojali kila mmoja bila kubagua kwa namna yoyote. Mchango na ushauri wako ni wa thamani kubwa kwetu. Mabadiliko tunayoyataka katika jamii kwa pamoja tukishirikiana yatawezekana.

4.Tunavumbua na kuviendeleza vipaji vya wanafunzi ili baadae viwasaidie hasa katika kuajiriwa na kujiajiri.
Tunakukaribisheni WINNING SPIRIT HIGH SCHOOL