Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya michezo mbalimbali inayochezwa na timu za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Aidha timu ya bunge la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) nayo ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo.

Michuano hii itakayofanyika kwenye viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Disemba mosi hadi 11/ 2017 yatahusisha michezo ya soka, mpira wa pete, wavu, gofu, kuvuta kamba, riadha na kutembea kwa mwendo kasi.