Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury amesema atapenda kupigana na mtu mwenye jina kubwa iwapo atarejea uwajani.

Fury mwenye miaka 29 tayari ameshasaini mkataba na kampuni ya MTK akijiandaa kumaliza adhabu yake. Anatarajia kusikiliza uamuzi wa mahakama mwezi Desemba dhidi ya kesi yake ya matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni mwaka 2016.

Chama cha ndondi nchini Uingereza kimesema bingwa huyo ambaye alipata mikanda ya IBF, WBA na WBO kwa kumchapa Wladimir Klitschko Novemba 2015, hatopewa leseni ya kupigana mpaka pale mambo yote yatakapowekwa sawa.