Siku chache baada ya Droo ya upangaji wa makundi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018, Urusi ambao ni waandaaji wametangaza kuwa viwanja vitano kati ya 12 vitakavyotumika, vimekwishakamilika.Viwanja hivyo ni Spartak wa Moscow, uwanja wa Fisht mjini Sochi, Uwanja wa mji wa Kazan, uwanja mkongwe wa Saint Petersburg Stadium na uwanja wa Luzhniki wa Moscow.

Kamati kuu ya kitaifa ya maandalizi imeahidi kuwa viwanja saba vilivyosalia, vipo katika hatua ya mwisho ya umaliziaji mdogo.