Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia amemsimamisha kazi Afisa usafirishaji wa jiji, Edward Mariko kwa makosa ya uzembe kazini ya kuto wajibika kwa wakati katika nafasi yake na kusababisha Magari zaidi ya mawili kupata ajali na kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mkurugenzi huyo kufanya ziara ya kushtukiza katika karakana ya halmashauri hiyo na kubaini kuwepo kwa makosa hayo ambayo yamekuwa yakijurudia kwa afisa huyo licha ya kupewa maonyo kadhaa ya kinidhamu.

Aidha Mkurugenzi amemteua, Bw Frank Sanga kukaimu nafasi hiyo huku utaratibu wa kumwajibisha Afisa usafirishaji huyo zikifuata kueleza ni kwanini ameingizia hasara halmashauri kwa kushindwa kutoa taaarifa ya magari kupata hajali ikiwemo pia uzembe wa kusimamia madereva kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Afisa usafirishaji alimueleza mkurugenzi kuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake kutokana na madereva kutoa taaarifa za uwongo na muda mwingine kuchelewa kufikisha taaarifa ya malalamiko kwake na sio kwamba ni uzembe yeye kusimamia ofisi yake.