Na Michael Nanyaro

Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mh Juma Aqweso amezitaka taasisi za serikali zinadaiwa zaidi ya shs. bilioni 39 nchi nzima na mamlaka mbali mbali za  maji na usafi wa mazingira (MUWSA) kulipa deni hilo kwa wakati ili zisiwe chanzo cha kuzorotesha huduma za maji kwa wananchi…

Naibu waziri ametoa rai hiyo wakati alipozungumza na wafanyakazi wa (MUWSA) na kutembelea baadhi ya vyanzo vya maji na kuelezwa juu ya madeni hayo ya muda mrefu ambayo yanakwamisha maendeleo ya (MUWSA).

Mh Aqweso amesema, taasisi hizo hazina budi kufuata taratibu za malipo kabla hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi ya taasisi hizo huku jeshi la magereza likiwa limeonyesha ari ya kulipa baada ya kutangulza zaidi ya shs. 100mil/=

katika taarifa yake Mkurugenzi mtendaji wa (MUWSA) Bi Joyce Nsilu ameitaja baaadhi ya miradi ambayo inakwamishwa katika utekelezaji wake na taasisi hizo ni mradi mkubwa wa maji wa mang’ana ambao utahudumia kata mbili za Uru kusini na Uru kaskazini wilayani Moshi  kwa kuwa haipati ruzuku kutoka serikalini.