Wataalamu wa jiolojia wamesema kuwa tetemeko la ardhi limetokea Kata ya Aneti wilayani Chamwino usiku wa kuamkia jana lina ukubwa wa 5 katika kipimo cha richter.

Tetemeko lenye ukubwa wa 5.1 kipimo cha richter lilitokea Julai mwaka juzi katika kata hiyo na kusababisha nyumba zaidi ya 60 kupata nyufa. Ofisa Mwandamizi wa Jiolojia katika Wakala wa Jiolojia Nchini (GST), Gabriel Mbogoni alisema tetemeko hilo limetokea katika maeneo lilipotokea mwaka jana Kusini

Tulipoulizwa kama tetemeko hilo lililotokea saa 9 limeleta madhara yoyote, Mbogoni alisema hajapata taarifa.  Mbogoni alisema tetemeko linaweza likawa na ukubwa mdogo lakini likaleta madhara kutegemea na mpasuko wa miamba umetokea katika kina gani.

 

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga alisema hadi jana mchana kulikuwa hakujaripotiwa madhara yoyote.  Tetemeko kubwa la ardhi kutokea nchini lilitokea miaka tisa iliyopita katika eneo la Oldonyo Lengai ambalo lilikuwa na ukubwa wa 5.9 kwa kipimo cha richter.