Wataalamu wa sekta ya mifugo nchini wamesisitizwa kuandaa mikakati itakayoweza kuja na majawabu ya utatuzi wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji nchini.

Aidha licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi ya nyama lakini bado bei ya nyama ipo juu kwenye mabucha mbalimbali huku baadhi ya wananchi wakishindwa kumudu kula nyama ya ng’ombe.

Hayo yamesemwa jana Jijini hapa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati alipokuwa akizungumza mkutano wa siku tatu wa Wataalamu wa Mifugo kutoka nchi mbalimbali za Afrika

Naye Profesa, Dominic Kambarage ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo (TVA) alisema wataunda kamati maalum itakayoshirikisha wataalam mbalimbali wa mifugo na uvuvi ili kubainisha matatizo ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kutatua matatizo yanayotokea mara kwa mara.