Maelfu ya raia katika miji tofauti nchini Uturuki yaandamana kupinga na kukemea uamuzi  uliochukuliwa na Donald Trump kutambua jii la Jerusalemu kama mjini mkuu wa Israel.

Maandamano makubwa yameshuhudiwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Ankara na balozi ndogo inayopatikana mjini Istanbul.

Mashirika tofauti ya kiraia ikiwemo shirika la vijana la Anatolia yameshiriki katika maandmano hayo.

Waandamanaji waliokutana katika mskiti wa Fatih mjini Istanbul  wametoa wito wa umoja kwa waislamu kupinga uamuzi huo.

Maandamano yameripotiwa mkoani Konya, Bursa, Antalya, Muğla, Manisa, Adana, Bartin, Karabuk, Samsun, Yozgat, Malatya, Gaziantep, Kahramanmaras, Şanliurfa, Şirnak na Diyarbakir.