Nigeria yambadilisha kamanda wa kupambana na Boko Haram

0
23

Nigeria imeamua kumbadilidhsa kamanda wa jeshi anayeongoza vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram ikiwa imepita nusu mwaka tu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, wimbi la mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram limeongezeka sana hivi sasa, hivyo jeshi limeamua kumbadilisha kamanda aliyekuwa anaogoza vita dhidi ya genge hilo.


Wanamgambo wa Boko Haram

 

Makamanda wa kijeshi huwa wanabadilishwa mara kwa mara kama njia ya kutoa msukumo mpya katika vita dhidi ya ugaidi kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo uasi wa genge la wakufurishaji la Boko Haram umeingia katika mwaka wake wa tisa. Kuzuka wimbi jipya la mashambulizi ya Boko Haram kunaonesha namna Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alivyoshindwa kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais.

Msemaji wa Jeshi la Nigeria amesema kuwa, Kamanda Ibrahim Attahiru aliyekuwa anaongoza vita dhidi ya Boko Haram amebadilishwa na nafasi yake itachukuliwa na Meja Jenerali Rogers Nicholas.

Miongoni mwa mashambulizi yaliyotokea katika kipindi cha Ibrahim Attahiru ni pamoja na kutekwa nyara timu ya maafisa wa mafuta, utekaji nyara ambao ulipelekea watu 37 kuuawa mwezi Julai mwaka huu. Mashambulizi mengine makubwa ya Boko Haram yaliyotokea katika kipindi cha ukamanda wa Attahiru ni yale ya miji ya Magumeri, Biu na Madagali.

Wimbi hilo jipya la mashambulizi ya Boko Haram limeuweka chini ya alama ya kuuliza uwezo wa serikali ya Muhammadu Buhari ambaye aliahidi kuwaangamiza kikamilifu magaidi wa Boko Haram mara atakapochaguliwa kuwa rais wa Nigeria. Hata jeshi lililoundwa na nchi za Cameroon, Niger, Chad na Nigeria limeshindwa kukabiliana na wimbi la mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram.