Bingwa wa ndondi za kulipwa barani Afrika Francis Cheka anatarajia kupanda ulingoni Desemba 16 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona kuzichapa na Shabani Kaoneka. Kaoneka anagombea mkanda wa OBO Afrika ambao Cheka anaushikilia kwa miaka mitatu tangu auchukue.

Cheka amesema ujio wa mpambano huo katika mkoa wa Mtwara ni kukuza na kuendeleza mchezo wa ngumi kwa mkoa wa Mtwara na mikoa ya kusini kwa ujumla na kuutangaza mkoa kitaifa na kimataifa.

Pia, mchezo huo utakuwa na mapambano ya utangulizi ambayo yatashirikisha mabondia wa mkoa wa Mtwara na mikoa jirani ya ukanda wa kusini ili kujitangaza na kuwahamasisha kucheza mchezo huu kama fursa ya kujipatia pesa kwani ni kazi kama kazi zingine na kuwafanya vijana kujiajiri kupitia mchezo wa ngumi.