Mtoto wa Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu Seya’ Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu baada ya Rais John Magufuli kutangaza familia yao ipo huru kuanzia leo Jumamosi. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika.

Michael Nguza ambaye hivi sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela amesema : “Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa baadaye. “Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano haya familia naomba kuweni wavumilivu,” amesema Nabii Michael.