Mbunge wa Jimbo la Siha, Dk. Godwin Mollel kwa tiketi ya (CHADEMA) ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kutangaza nia ya kuhamia CCM.

 

Katika Taarifa yake Mbunge huyo amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuonesha uzalendo wa kweli kwani haoni sababu ya kuendelea kumpinga mtu ambaye anatekeleza kila alichokuwa akikipigania akiwa upinzani.

 

Amedai kuwa dhamira yake imekataa kuukataa ukweli kuwa ana wajibu wa kushirikiana na Rais Magufuli kupigania rasilimali za nchi badala ya kuendeleza siasa za kubishana hata na ukweli ambao yeye anauona.

 

Akizungumzia jinsi alivyopokea taarifa hiyo, Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini AMANI GOLUGWA amesema, chama chao kimepokea taarifa hizo na kinaamini kuwa kuna chanzo kinachopelekea hali ya kuhama hama ila ipo siku kitajulikana wazi.