Kufuatia ushindi wa magoli 4-0 iliopata jana dhidi ya Swansea City, Klabu ya Manchester City imefanikiwa kuvunja rekodi iliyodumu kwa takribani miaka 15 ya ushindi mfululizo kwenye mechi za ligi kuu ya nchini Uingereza.

Kwa ushindi huo City sasa imeshinda mara 15 na kuipiku Arsenal iliyowaweka rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo mwaka 2002.

Katika mechi ya jana magoli ya Man City yalifungwa na David Silva aliyefunga mawili, Kevin De Bruyne na Sergio Aguero wakifunga moja kila mmoja, na kuifanya timu hiyo ifikishe alama 49 kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.