Chama cha mpira wa miguu cha Uingereza FA kimempa hadi jumatatu ijayo kocha wa manchetser united kuhusiana na baadhi ya matamshi aliyotatoa kabla ya mechi baina ya timu yake na vinara wa vinara wa ligi kuu ya soka ya nchi hiyo Manchester City.

Miongoni mwa kauli ambazo zinadaiwa kuwa si za kiuanamichezo, Mourinho alitamka kuwa wachezaji wa wajitahidi kuingia uwanjani bila kulegea, wasijiangushe angushe kama desturi yao ili kusubiri upendeleo wa mwamuzi.

Nyingine ni pale alipotamka kuwa yeye hapewi uhuru kama ilivyo kwa makocha wengine kuzungumza chochote kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya siasa akimtolea mfano wa wazi Pep Guardiola kwamba hakuzuiwa kuvaa kiwambo cha njano kuunga mkono kura za maoni za Katalunya.

Kufuatia hayo na mengine mengi, FA imemtaka Mourinho kujitetea hadi kufikia Jumatatu saa kumi na mbili jioni kwa saa za Uingereza.