Timu ya taifa ya Rwanda (amavubi) inatarajiwa kusafiri kwenda hadi nchini Tunisia kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani CHAN yatakayofanyika nchini Morocco kuanzia januari 12 hadi Februari 4.

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu la Rwanda FERWAFA, Vincent Nzamwita amesema kikosi cha timu hiyo kitaanza kambi hiyo ya mazoezi Januari 2 hadi januari 11 ambapo pia kitacheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki.

Kocha mkuu wa timu, Antoine Hey ameishukuru Ferwafa kwamba imetoa fursa nzuri kwa wachezaji wake kupata uzoefu ili kwenda sambamba na mashindano yenyewe.

Rwanda iko kundi C la mashindano hayo pamoja na timu za Libya, Nigeria na Equatorial Guinea.