Aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi, PC George Bisongoza (30), aliyefukuzwa kazi mwaka 2013, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kusafirisha magunia 18 ya bangi.

PC George na mwenzake, walikamatwa usiku katika eneo la Kilema Pofu barabara ya Moshi-Himo, wakisafirisha bangi hiyo kwa kutumia gari la polisi, Toyota Landcruicer.

Hukumu ya kifungo hicho cha maisha, imetolewa leo Ijumaa Desemba 15 na Benard Mpepo ambaye ni Hakimu Mkazi mwandamizi mwenye mamlaka ya nyongeza ya kusikiliza kesi kama Jaji.

Akisoma hukumu hiyo katika Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, Mpepo amesema ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, haukuacha shaka dhidi ya mshtakiwa kutenda kosa hilo.