Sam Timbe kutoka Uganda ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Tusker FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini Kenya akichukua nafasi iliyoachwa wazi na mganda mwenzake George Nsimbe na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili.

Hii ni mara ya pili kwa Sam kufundisha klabu za Kenya,akiwa amewahi kuifundisha kwa mafainikio Sofapaka kabla ya kujiuzulu kutokana sintofahamu ya malipo.

Katika kibarua chake hicho kipya, Sam atasaidiana na Francis Baraza pamoja na Leonard Odipo.