Aliyewahi kugombea ubunge wa jimbo la Ilala 2015 kwa tiketi ya CHADEMA na mjumbe bodi ya wadhamini wa chama hicho Muslim Hassanali,Ajitafakari kwanza ndipo  kuhamia CCM

”Haikuwa kazi rahisi kuchukua maamuzi ya kuihama CHADEMA na kujiunga CCM, Ila imebidi niweke maslahi yangu binafsi pembeni na kujiunga CCM ili nipambanie nchi yangu

Kwa muda wa mwaka mmoja nimijitafakari sana na sasa nimmeamua kumuunga mkono mhe. Magufuli kwa kupigania nchi yangu. Kuna vitu tulikuwa tunapigia kelele na CHADEMA kama mikataba ya madini ambapo leo sina haja ya kupiga kelele kutokana na anayoyafanya Rais na Serikali. Pia na utumiaji mbaya wa madaraka lakini kwa utawala huu wa Magufuli watu wanapata imani

Nimekosoa Serikali vya kutosha ila sasa ni muda wa kushirikiana nayo, sio wakati wa kuikosoa serikali na kuichafulia jina

Sijawahi kuwa mwana CCM tangu nimezaliwa lakini leo najisikia faraja kujiunga na kundi kubwa na wanachama wa CCM”