Bunge la Misri limetangaza kurefusha muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu mingine ambao ulianza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kujiri mashambulizi makubwa katika makanisa ya Wakristo wa Kikopti nchini humo.

Hatua hiyo ilichukuliwa jana na bunge la Misri kufuatia pendekezo lililotolewa na Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo. Hali ya hatari ilianza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka jana nchini Misri kuafutia kujiri mashambulizi mawili makubwa katika makanisa ya Wakristo wa Kikopti katika miji miwili ya Tanta na Alexandria kaskazini mwa Misri ambapo watu 45 walipoteza maisha.


Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri   

Muda wa hali ya hatari uliongezwa kwa mara kadhaa huko Misri baada ya kujiri mashambulio hayo. Kurefushwa muda wa hali ya hatari kunawazidishia uwezo mkubwa polisi wa nchi hiyo katika oparesheni za utiaji mbaroni na kusimamia amani, hatua ambayo imetajwa na makundi ya kisiasa kuwa inabana uhuru wa harakati.