NA, MICHAEL NANYARO

Naibu waziri wa fedha na mipango,Dr Ashatu kijaji amewataka wafanyabiashara mkoani Arusha kuacha matumizi ya fedha za kigeni wawapo ndani ya nchi na kusema kuwa wizara hiyo ipo katika mkakati wa kurekebisha sheria ya fedha za kigeni pamoja pia na Benki ili kukabiliana na mzunguko wa fedha za kigeni ndani taifa.

Hilo linakuja zikiwa zimepita siku chache tanguRais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kutoa agizo hilo,ambapo Dr Kijaji ametoa agizo hilo hii leo katika kikao maalumu na wafanyabiashara jijini Arusha ambapo amesema kuwa chanzo kikubwa cha shilingi ya Tanzania kuzidi kushuka ni kutokana na matumizi ya fedha za kigeni.

Wakati Naibu waziri huyo akitoa agizo hilo,awali Meneja wa Mamlaka ya mapato katika mkoa wa Arusha alitoa agizo kwa wafanyabiashara hao kuhakikisha wanaendelea kulipa mapato kwani hakuna nchi inayoweza kujiendesha bila mapato.

Aidha kwa upande wake mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia,amesema jiji hilo limejipanga katika suala la ukusanyaji mapato pamoja pia na kupunguza msongamano ndani ya jiji hilo ikiwa ni pamoja na kuanzisha stand ya mabasi katika eneo la Moshono.