Jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu na kufikia matukio 1963 mwaka 2017 ukilinganisha na makosa 2817 ya mwaka 2016.

Aidha amesema kuwa matukio ya ubakaji na ulawiti yameongezeka na kufikia 149 katika kipindi cha mwaka 2017 ukilinganisha na makosa 144 ya mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mwaka ya hali ya ulinzi na usalama kwa mkoa wa Arusha JANA,  kamanda wa Polisi mkoani hapa,Charles Mkumbo amesema kuwa kuongezeka kwa matukio hayo ni kutokana na malezi mabaya ya wazazi yanayotokana na mmomonyoko ywa maadili .

Aliongeza kuwa sababu nyingine ni msukumo unaotokana na imani za kishirikina na  tamaa za kupata Mali kwa njia potofu.

Akizungumzia takwimu za matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha amesema kwamba katika kipindi cha mwaka 2016 makosa hayo yalikuwa 15 huku mwaka 2017 yakipungua na kufikia makosa mawili tu.