Wamiliki wa radio hususani radio za kijamii wameombwa kuendelea kuboresha vipindi vyao ili kuifikishia jamii ujumbe wenye maudhui na wenye kuelimisha ili kuleta maendeleo katika jamii.

Hayo yamebainishwa na mkuu idara ya utangazaji kutoka katika mamlaka ya mawasiliano Tanzania Tcra Injinia Andrew Kisaka wakati alipokuwa akizungumza na Channel ten kuhusiana na maadhimisho ya siku ya radio duniani ambapo amesema radio za kijamii zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kwa jamii hususani katika kuelimisha na kuchochea maendeleo kwa jamii.

Injinia Kisaka amesema mpaka sasa kuna radio 6 tu za kijamii nchini na kutoa wito wa kuanzisha radio nyingi za kijamii kwa ajili ya kuwafikia watanzania wengi zaidi na kutoa ujumbe wa kuelimisha .

Kwa upande wao baadhi ya watangazaji wa radio wanazungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika radio.

Siku ya radio duniani huadhimishwa kupitia Shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni Unesco kila februari 13 duniani kote .