Katika michezo ya olimpiki ya majira ya baridi inayoendelea nchini Korea Kusini, mchezaji Jiayu Liu kutoka China ameshinda medali ya fedha katika kipengele cha kuteleza kwenye korongo lililochongwa kwa muundo wa nusu bomba.

Jiayu alishinda zawadi hiyo kutokana na kushika nafasi ya pili nyuma ya Chloe Kim wa Marekani ambayo alishinda medali ya dhahabu.

Katika michuano hiyo inayoingia siku ya sita leo, timu ya taifa ya Ujerumani ndiyo inaongoza kwa kuwa na medali nyingi za dhahabu, 5 ikifuatiwa na Uholanzi yenye 4